ARGENTINA YAITUNGUA COLOMBIA KWA MATUTA …Teves aibuka shujaa, sasa huenda ikavaana na Brazil nusu fainali
Carlos Teves amefunga penalti ya ushindi wakati Argentina ikiifunga Colombia kwa penalti na kutinga nusu fainali ya Copa America.
Argentina walitawala mpira kwa muda wote wa mchezo lakini kipa David Ospina alikuwa kikwazo kwao kwa kuondoa michomo mingi ya hatari ikiwemo ya Sergio Aguero, Lionel Messi na Nicolas Otamendi.
Hiyo ikamaanisha kuwa penalti zinahitajika na baada ya Jeison Murillo wa Colombia kupoteza penalti yake, Tevez akafunga na kuipa Argentina ushindi wa 5-4.
Argentina sasa itakabiliana na mshindi wa usiku wa kuamkia kesho kati ya Brazil na Paraguay kwenye nusu fainali itakayopigwa Jumanne.
Ushindi huu ni kumbukumbu nzuri kwa Teves ambaye alitokea benchi na kuibuka shujaa kwa nchi yake.
Kukiwa hakuna 'extra time' katika hatua za robo fainali na nusu fainali za Copa America, mchezo ukaenda hatua ya penalti baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya 0-0.
Jumla ya penalti 15 zikapigwa, tano zilipotea kwa kutoka nje au kuokolewa kabla Teves hajamaliza mchezo.
Tevez akimtungua kipa Ospina kwa penalti iliyoipa ushindi Argentina
Tevez akisubiriwa na kipa wake Sergio Romero - ambaye aliokoa penalty ya Juan Camilo Zuniga
Teves akishangilia na kipa wake
Wachezaji wa Argentina wakishangilia baada ya Carlos Tevez kufunga penalti ya ushindi kwenye nusu fainali ya Copa America
Comments
Post a Comment