- Get link
- X
- Other Apps
ARDA TURAN ameripotiwa kwamba anataka kuondoka Atletico Madrid haraka iwezekanavyo, na kuzialika klabu zinazomtaka kufanya taratibu za uhamisho hata kesho, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu zilizo kwenye mazungumzo ya kumsajili.
Kiungo huyo mchezeshaji raia wa Uturuki, anajiandaa kuondoka Madrid kiangazi hiki, ambapo tayari imethibitishwa kuwa wakala wake kwa sasa anahangaikia safari yake ya kuondoka La Liga.
Kwa mujibu wa gazeti la AS la Hispania, klabu za PSG, Chelsea na United tayari zinafanya mazungumzo na wawakilishi wa Turan mwenye umri wa miaka 28.
"Arda ameshinda kila kitu akiwa na Atletico ndani ya miaka minne na sasa ni wakati wa kutafuta changamoto mpya"Ahmed Bulut
Wakala wake Ahmed Bulut mara kadhaa amekuwa akisema kuwa Turan angependelea kwenda England ingawa AC Milan na PSG nao wamekuwa wakimnyatia.
Bulut ameiambia NTVSpor: "Arda ameshinda kila kitu akiwa na Atletico ndani ya miaka minne na sasa ni wakati wa kutafuta changamoto mpya".
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment