Beki wa Chile Gonzalo Jara amefungiwa baada ya kumtia            dole mshambuliaji wa Uruguay Edinson            Cavani kwenye mchezo wa robo fainali ya Copa America.
        Jara alinusurika kupewa adhabu na mwamuzi            wakati Cavani akilambwa kadi nyekundu baada ya kuhamaki na            kumsukuma beki huyo. 
        Ushahidi wa picha umemtia hatiani Jara na            sasa atakosa michezo yote iliyosalia hata kama Chile itasonga            mbele hadi fainali.
        Jara alimlamba kofi la kishkaji Cavani            kabla ya sekunde chache baadae hajamtia dole mshambuliaji huyo            wa PSG.
        Cavani  alihamaki, akamsukuma kidogo Jara            ambaye alikuwa mwepesi kuzuga na akajitupa chini. Cavani             akapewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
        Kutolewa kwa Cavani dakika ya 63            kuliiathiri Uruguay iliyojikuta inafungwa bao pekee dakika ya            81.
          
                              
        Hili              ndio dole lililoleta balaa
        Edinson Cavani (watatu              kushoto) akilalamika baada ya kuzinguliwa Gonzalo Jara 
        Jara anamsogelea Cavani              na kumpiga dole
        Jara anajiangusha na              kumsababishia kadi nyekundu Cavani
        Cavani analambwa kadi              nyekundu
        
Comments
Post a Comment