ALEXANDRE LACAZETTE AENDELEA KUITOA UDENDA MANCHESTER UNITED


ALEXANDRE LACAZETTE AENDELEA KUITOA UDENDA MANCHESTER UNITED

MANCHESTER UNITED bado inapambana kwa nguvu zote kuweza kukamilisha uhamisho wa mpachika mabao nyota wa Lyon ya Ufaransa, Alexandre Lacazette.
Mashetani hao wekundu wamevutiwa zaidi na uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu ulioonyeshwa na mshambuliaji huyo msimu huu, ambapo alitikisa nyavu za adui mara 32.
Straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliyeibuka kinara wa mabao katika Ligue 1, anafukuziwa na klabu kadhaa barani Ulaya.
Kwa mujibu wa mtandao wa FIchajes.net, Lacazette atatangaza uamuzi juu ya mustakabali wake wiki ijayo baada ya kumaliza mapumziko ya mwisho wa msimu.


Comments