JASPER CILLESSEN yuko huru kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United baada ya klabu yake ya Ajax ya Uholanzi kukubali kumpiga bei.
United inaaminika kumfanya Cillessen moja ya malengo yao makubwa wakati ikitafuta mbadala wa kipa wake namba moja, David De Gea aliye njiani kujiunga na Real Madrid.
Habari za awali zilidai kuwa Ajax ilikataa dili la kumuuza Cillessen, lakini sasa klabu hiyo inaelezwa kuwa na furaha kumwachia kipa huyo kuhamia Old Trafford.
United inatakiwa kulipa pauni 17.8 kuweza kumaliza biashara, pesa ambayo iko ndani ya uwezo wao.
Comments
Post a Comment