Mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand ametangaza rasmi kustaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu huu akiwa na Queens Park Rangers.
Uamuzi wa Ferdinand kutundika daluga umekuja baada kifo cha ghafla cha mkewe kilichotokea mwanzoni mwa mwezi Mei.
Sentahafu huyo mwenye umri wa miaka 36 ametangaza uamuzi huo 'live' kupitia BT Sport na muda mfupi baadae akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuwashukuru wote waliompa pole baada ya mkewe Rebecca aliyekuwa akisumbuliwa na kansa kufariki na kumwachia watoto watatu.
Rio Ferdinand ametangaza kuachana na soka
Ferdinand aliiongoza Manchester United kushinda taji la Champions League dhdi ya Chelsea Mei 2008
Ferdinand akiwa na mkewe Rebecca ambaye alifariki mwezi Mei mwaka huu kwa maradhi ya kansa
Ferdinand akipozi na mkewe Rebecca katika sherehe za kufunga msimu za wa mwaka 2013 za Manchester United
Rebecca amemwachia Ferdinand watoto watatu - Lorenz, Tate na Tia
Rio Ferdinand akiwa na Manchester United Mei 2003, ameshinda mataji sita ya Premier League katika muda wake aliokaaa Old Trafford
Ferdinand akipozi na kocha wa enzi hizo wa Manchester United Sir Alex Ferguson wakati akisajiliwa mwaka 2002
Comments
Post a Comment