WAKALA WA RAHEEM STERLING AWAPA MAKAVU LIVERPOOL ...awaambia mchezaji hawezi kusaini mkataba mpya hata akilipwa laki 9 kwa wiki
Raheem Sterling hawezi kusaini mkataba mpya Liverpool hata kama atalipwa pauni 900,000 kwa wiki, wakala wake Aidy Ward amefunguka.
Ward anategemea mchezaji wake atatua Manchester City au Chelsea huku akifutilia mbali uwezekano wa Raheem kujiunga na Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich.
Wakala huyo pia amewashambulia machambuzi wa soka akiwemo mchezaji wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher.
Ward (pichani juu kushoto) aliliambia gazeti la Evening Standard: "Sijali mahusiano na klabu wala hali ya klabu. Sijali.
"Kwa hakika hatasaini. Hawezi kusaini kwa pauni laki 7, 8 au hata 9 kwa wiki. Hawezi kusaini.
"Wajibu wangu ni kuwafanyia kazi nzuri (wateja wangu). Kama watu wanasema mimi ni mbaya kwenye kazi yangu au wanashauriwa vibaya, haijalishi chochote kwangu.
Aidy Ward (kushoto) awapasua vichwa Liverpool
Comments
Post a Comment