Vipaji ‘kibao’ vyaonekana UMISETA ikianza kutimua vumbi Dar


Vipaji 'kibao' vyaonekana UMISETA ikianza kutimua vumbi Dar

???????????????????????????????

Mashindano ya Umoja wa Michezo wa shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yameanza leo kwa mkoa wa Dar es Salaam yakifanyika kwenye viwanja vya nje vya Taifa kwa ushirikisha shule za wilaya zote za mkoa huo (Kinondoni, Ilala na Temeke) ili kutafuta timu moja ya Kanda ya Dar es Salaam itakayokwenda kupambana kwenye michuano ya UMISETA  ngazi ya Taifa itakayofanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 8 hadi Juni 21 mwaka huu.

Michuano hiyo inayoshirikisha michezo yote yaani mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, riadha, kuruka viunzi, kuruka chini, kurusha kisahani na mingine mingi ambayo tayari ilianza kusahaulika kwenye sekta ya michezo kwa upande wa Tanzania.

???????????????????????????????

Mratibu wa mashindano hayo Abel Mtweve amesema, mashindano hayo ambayo yameanza leo, yataendelea kesho na keshokutwa yatafikia tamati huku akiongeza kuwa, walimu wamekuwa wakipata changaoto kubwa katika kuchagua majina ya wanamichezo watakaounda timu ya Kanda ya Dar es Salaam kutokana na wachezaji wengi kuwa na vipaji.

"Michuano hii imeanza leo lakini itaendelea tena kesho na keshokutwa itakuwa mwisho. Baada ya mashindano tunatarajia kuwa na timu moja kwa michezo yote ambayo itakwenda Mwanza kwa ajili ya mashindano kama haya lakini kwa ngazi ya Taifa", amesema Mwinuka.

"Tumekuwa na wakati mgumu hasa katika kuchagua majina ya vijana ambao wataunda timu ya Kanda kutokana na wachezaji wengi kuonesha vipaji vya hali ya juu kwenye kila mchezo.", Mwinuka aliongeza.

"Tunatarajia kuondoka Dar es Salaam Juni 6 kuelekea Mwanza, Juni 7 tutafanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa na michuano hiyo ambapo itaanza rasmi Juni 8 mpaka itakapomalika Juni 21mwaka huu", alimaliza Mwinuka.

Serikali imerejesha michezo shuleni baada ya kuifuta kwa muda mrefu michezo hiyo. Kurudi kwa michezo hiyo kumetokana na wadau wa michezo kupigia kelele uamuzi wa serikali kufuta michezo kwenye ngazi ya shule hali iliyopelekea timu za taifa kuboronga kwenye michuano ya kimataifa.



Comments