Louis van Gaal ameonya kuwa atakubwa 'bize' ile mbaya pindi dirisha la usaliji litakapofunguliwa mwezi ujao ambapo amepania kusajili wachezaji mahiri watakaoleta uwiano wa timu.
Van Gaal ambaye ana jueri ya kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya usajili, amesema wachezaji wapya wataingia na wengine wataondoka Old Trafford.
Kauli hiyo inazidi kutia mashaka juu ya uwepo wa kipa David de Gea ambaye anatakiwa na Real Madrid.
"Chaguo letu halikukidhi uwiano wa timu - tumefanikiwa kushika nafasi ya nne lakini tunapaswa kujipanga ili tuwe mabingwa," alisema Van Gaal.
"Tunalazimika kuboresha chaguo letu, nitakuwa 'bize' kuangalia wachezaji wengi dirisha la kiangazi na nadhani timu kama Manchester United inastahili kufanya hivyo," aliongeza.
Aidha, Van Gaal amemtaja De Gea kama mchezaji wake bora wa msimu.
Boss wa Manchester United, Louis van Gaal anataraji kufanya usajili wa kishindo
Van Gaal alikuwa akizungumza katika sherehe kutoa tuzo kwa wachezaji wa Manchester United
Comments
Post a Comment