Van Gaal anyosha mikono kumbakiza De Gea


Van Gaal anyosha mikono kumbakiza De Gea

_65524053_david-de-gea-getty

Kocha  wa Manchester United, Louis van Gaal amekiri kuwepo ugumu wa kumzuia  mlinda mlango wa klabu hiyo, David De Gea kujiunga na Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu, licha ya mashetani wekundu kumpa ofa nzuri ya kandarasi mpya.

Van Gaal anaamini  ni vigumu kwa De Gea kukataa ofa ya kujiunga na klabu kubwa duniani ya Real Madrid kwasababu yeye ni Mhispania, mpenzi wake ni Mhispania na wazazi wake wanafika England kila juma kumsalimia Mlinda mlango huyo, hivyo ni rahisi kushawishika kurudi nyumbani.

De Gea amepata majeruhi katika sare ya 1-1 waliyopata Man united jana Old Trafford dhidi ya Arsenal na nafasi yake ikachukuliwa na Victor Valdes  dakika ya 74, lakini mashabiki wa Manchester United kwa dakika zote 90 walishikilia mabango yenye ujumbe wa kumuomba Mhispania huyo aendelee kubaki Old Trafford.



Comments