Boss wa Manchester United Louis Louis van Gaal amemtaka Angel di Maria aliyenununuliwa kwa pauni milioni 60 kukaza buti vinginevyo atapigwa bei.
Ni wazi kuwa sasa uvumilivu unafika ukingoni kwa Van Gaal ambapo amemtaka winga huyo kubadilika na kuendana na mfumo wa timu.
Di Maria alinunuliwa kiangazi kilichopita kutoka Real Madrid kwa rekodi mpya ya klabu, lakini amekuwa mmoja wa wachezaji 'mizigo' Old Trafford.
Van Gaal amesema: "Wachezaji wanapaswa kuendana na mfumo wa uchezaji wa timu na Di Maria ni alizima awe hivyo.
"Je Di Maria anaweza kujifunza? Hilo ni jambo la kusuburi na kuona kitakachotokea. Anapaswa kucheza kwa namna tunavyotaka. Siyo namna ninavyotaka mimi bali ni kwa namna sisi kama klabu tunavyotaka".
Angel di Maria anapaswa kupigania nafasi yake Old Trafford
Di Maria amefunga mabao matatu tu Premier League tangu alipojiunga na United kwa £60m kutoka Real Madrid
Comments
Post a Comment