Usajili wa Kaseke, Mwinyi, Tinocco watosha Yanga, TFF wakwamisha mipango ya kimataifa….



Usajili wa Kaseke, Mwinyi, Tinocco watosha Yanga, TFF wakwamisha mipango ya kimataifa….
DSC_9372
MABINGWA wa soka Tanzania bara, Young Africans wametangaza kumaliza usajili wa wachezaji wa ndani na sasa wanaangalia wa kimataifa.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroa amesema wachezaji wa ndani waliowasajili mpaka sasa wanatosha na wanachosubiri ni majibu kutoka TFF juu ya mapendekezo waliyowasilisha wakiomba kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni.
Yanga wamependekeza usajili wa wachezaji wa kigeni angalau ufikie idadi ya wachezaji nane (8).
"Wachezaji wa ndani tuliosajili wanatosha, sasa hivi kinachotukwamisha kidogo ni kauli kutoka kwa wenye mpira nchini TFF juu wachezaji wangapi wa kigeni tunaruhusiwa kusajili". Amesema Dr. Tiboroa na kuongeza: "
 "Malengo yetu mwaka huu ni kuongeza uzoefu kidogo kwa maana ya kupata wachezaji wengi wa nje na kutengengeza kikosi imara zaidi ya kile kilichopita".
Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji watatu wa ndani ambao ni kiungo mshambuliaji kutoka Mbeya City fc, Deus Kaseke, mlinda mlango kutoka Kagera Sugar, Benedictor Tinocco na mlinzi wa kushoto Mwinyi Hajji kutoka KMKM.


Comments