Mkutano Mkuu wa Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umefanyika leo Jumapili na kupitisha maazimio ya kuiondoa madarakani Kamati tendaji na Sekretarieti yake ikiwa ni pamoja na kumsimamisha Makamu Mwenyekiti wake na kuteua Sekretarieti mpya.
Kamati hiyo ya utendaji pamoja na Sekretarieti yake walishindwa kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya Klabu ya Toto Africans kwa kipindi cha mwaka mmoja 2014-2015 na yale yote yaliyojiri katika mchakato wa kuelekea Ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo humo inasemekana kuwa kulikuwa na ufujaji mwingi wa fedha na matumizi binafsi zaidi ya matumizi ya kawaida ya klabu kutoka fedha za wawezeshaji sanjari na vyanzo vya uwekezaji vya klabu.
Mapema leo Uongozi, Kamati na Sekretarieti iliyosimamishwa ilishindwa kuhudhuria mkutano huo bila kutoa sababu na hata maandalizi ya mkutano kama yalivyo agizwa hayakufanywa ambapo awali mkutano ulikuwa umepangwa kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji badala yake wanachama wakaamua mkutano huo ukafanyike kwenye eneo la wazi uwanja wa Nyamagana Mwanza.
Shaffihdauda.com Imefanya mazungumzo na Isaac Wakuganda ambaye ni msemaji mpya wa klabu hiyo aliyeteuliwa leo na kusema kama ifuatavyo.
"Kikubwa ambacho kimeweza kuazimiwa katika mkutano wa leo ambao umeweza kudumu kwa muda mrefu kidog ni kwamba kwa kauli moja wameazimia kuusimamisha uongozi mzima wa kamati ya Utendaji na vile vile Sekretalieti yote ambayo ilikuwepo madarakani, lakini pamija na hilo vilee vile Mkutano huo wa wanachama umeazimia kubatilisha uamuzi wa wajumbe wa kamati ya Utendaji Godfrey Kyabulasani pamoja na Godfrey Mwanalelya ambao waliandika barua za kujiudhuru" Ameelezea Isaac Wakuganda.
"Lakini vile vile mkutano wa leo umeweza kuteua kamati ya muda ya watu watatu ambao watakuwa na jukumu zima la kufanya mchakato wa kuweza kuhakikisha haki inapatikana na mwisho wa Siku Toto Africans inakuwa klabu yenye mafanikio" Amefunguka Isaac Wakuganda.
Msemaji huyo wa klabu ya Toto Africa klabu ambaoyoni miongoni mwa zile timu nne ambazo zitashiriki ligi kuu msimu ujao baada ya kupanda daraja mwaka huu, ametaja majina ya ya wajumbe walioteuliwa kuunda kamati maalumu kuwa ni Isaac Mwanahapa ambaye ni Katibu mkuu, Abubakar Seilf ambaye atakuwa ni muweka hazina, pamoja na yeuye mwenyewe Isaac Wakuganda ambaye ni msemaji huku akisema kuwa wanaanza majuku yao muda huu.
"Kazi yao kubwa kwa sasa ni kuhakikisha taarifa hizi zinakwenda katika vyombo husika ikiwemo chama Cha Soka Nyamagana NDFA, Chama cha Soka mkoa wa Mwanza MZFA, bila kusahau kubisha hodi kwa ofisi ya mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki ijayo kwasababu ameonyeshania ya dhati kuhakikisha anao timu ya Toto inafikia mafanikio" Amesema Isaac Wakuganda.
Katika mkutano huu wa wanachama Wakuganda amesema kuwa walikubaliana tarehe 18 waweze kukutana ikiwemo ni pamoja na kupanga tarehe ya mkutano mkuu ambao utakuja na agenda nyingine za maendeleo ya klabu hiyo ambayo imerejea ligi kuu baada ya kushuka misimu iliyopita.
Shaffihdauda.com Ilitaka kujua hatma ya viongozi waliokuwepo madarakani ambao wamesimamishwa, Je. wanaruhusiwa kutinga kama wagombea?
" Hatma ya viongozi hao waliosimamishwa ni kwamba itaamuliwa na mkutano ambao utatangazwa baadaye na kamati hii ya muda, lakini kikubwa milango bado iko wazi kwasababu hawa ni viongozi ambao wamesimamishwa kwahyo bado wanahaki zote, kwahiyo utakapofika wakati mkutano mkuu pengine ni mkutano wa uchaguzi bado nafasi ipo kwao" Amesema mseji huyo wa klabu ya Toto Afrca Isaac Wakuganda.
SIKILIZA MWENYEWE ILIVYOKUWA
Comments
Post a Comment