Taifa Stars yafa mbele ya Swaziland Cosafa


Taifa Stars yafa mbele ya Swaziland Cosafa

stars_0

TIMU ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' imeanza vibaya michuano ya Cosafa baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Swaziland katika mechi ya michuano hiyo iliyomalizika usiku huu uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace, Afrika kusini.
Stars walifungwa goli hilo kutokana na makosa ya safu ya ulinzi hususani upande wa kushoto alikocheza Oscar Joshua.
Hata hivyo Stars walijitahidi kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi ambazo washambuliaji wake John Bocco, Mrisho Ngassa, Said Ndemla, Simon Msuva walishindwa kuzitumia vizuri.
Baada ya kichapo hicho, Stars wanarudi kujiwinda na mchezo wa pili utakaopigwa mei 20 mwaka huu katika uwanja huo huo dhidi ya Madagascar majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.
Swaziland wao watachuana na Lesotho katika mechi ya pili ya kundi B.
Michuano ya Cosafa itaendelea kesho kwa mechi mbili, Shelisheli watachuana na Zimbabwe majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika kusini sawa na saa 12:00 jioni kwa saa za Tanzania, baadaye majira ya saa 1:30 usiku kwa saa za 'Sauzi' sawa na saa 2:30 usiku kwa saa za Tanznaia, Namibia watakabiliana na Mauritius.



Comments