SUNDERLAND WAPAKI BUS NA KUITIBULIA ARSENAL ...VIJANA WA WENGER SASA MASHAKANI KUMALIZA NAFASI YA NNE ...pata picha kibao za mechi hiyo ya Ligi Kuu
Arsenal na Sunderland wametoshana nguvu katika mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa sare ya 0-0 kwenye dimba la Emirates Stadium.
Sare hiyo imetosha kwa Sunderland ambayo sasa imejihakikishia kubaki Ligi Kuu, hatua iliyomfanya kocha Dick Advocaat atoe chozi la furaha.
Kocha huyo wa Sunderland inabidi amshukuru kipa Costel Pantilimon ambaye aliokoa michomo mingi ya wazi huku Steven Fletcher akipoteza moja ya nafasi adimu kwa wageni baada ya kupaisha mpira akiwa katika eneo zuri la kufunga.
Sunderland walipaki bus kwenye lango lao wakionekana wazi kutafuta sare.
Kama Arsenal watapoteza mchezo wao wa mwisho na kisha Manchester United wakaifunga Hull City Jumapili, basi vijana wa Wenger wanaweza kujikuta wakimaliza katika nafasi ya nne.
Olivier Giroud akichuana na John O'Shea
Steven Fletcher wa Sunderland akikosa boa la wazi
Kipa Ospina wa Arsenal anapangua mpira ulipigwa na Fletcher
Santi Cazorla akichuana na Connor Wickham
Jack Wilshere akikabiliana na Defoe
Fletcher jino kwa jino na beki Laurent Koscielny
Aaron Ramsey akilambwa kadi ya njano na refa Anthony Taylor katika kipindi cha kwanza
David Ospina akiondosha hatari nyingine
Theo Walcott apiga shuti lakini kipa Pantilimon anaondoa
Sunderland right back Jones sticks a leg out to block Giroud's cross into the box from the left
Arsenal defender Per Mertesacker and Sunderland striker Danny Graham chase down a loose ball
Winga wa Sunderland Adam Johnson akikota mpira mbele ya Mesut Ozil wa Arsenal
Nahodha wa Sunderland O'Shea akimvuta jezi Giroud
Boss wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa hana la kufanya
Kocha wa Sunderland Dick Advocaat akitoa maelekezo
Comments
Post a Comment