MICHUANO ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 mwaka huu katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
Kuelekea katika michuano hiyo, kiungo mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars, Ibrahim Ajib 'Mido' amemshukuru kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic kwa kumuamini na kumpa nafasi iliyosababisha kocha wa Taifa Stars, Mholanzi, Mart Nooij amjumuishe kwenye kikosi kilichopo Afrika kusini.
'Kwanza napenda kutanguliza shukurani kwa mwenyezi Mungu. Pia napenda kutoka shukuruni zangu kwa kocha Goran (Kopunovic) aliyeniamini na kunipa nafasi mpaka nimefikia hapa nilipo". Ajib ameuambia Mtandao huu kutokea nchini Afrika kusini.
Pia nyota huyo kinda amesema anajipanga kutumia vyema nafasi ya COSAFA kufanya maajabu endapo atapata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Stars.
"Hapa nilipofikia sio mwisho, nikipata nafasi huku nilipo (Afrika kusini) nitafanya maajabu makubwa kwa uwezo wa Mungu". Amesisitiza Ajib.
Comments
Post a Comment