Gerrard akiwapungia mkono mashabiki huku akiaga kwa kipigo
GOLI la dakika 26′ kipindi cha kwanza la Adam Lallana liliashiria Liverpool watamuaga kwa furaha nahodha wao Steven Gerrard ambaye amecheza mechi ya mwisho uwanja wa Anfield dhidi ya Crstal Palace.
Lakini dakika ya 43′ katika kipindi hicho Jason Puncheon alisawazisha goli hilo na kuinyamazisha Anfield, huku kila shabiki akitafakari nini kitatokea katika siku hii kubwa kwa nahodha na kiongozi wa Liverpool, Gerrard.
Liverpool wakihaha kutafuta goli la kuongoza, Wilfried Zaha katika dakika ya 60′ akaifungia Palace goli la pili sekunde 22 tu baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi.
Marudio ya video yameonesha kama Zaha alikuwa ameotea kabla ya kufunga, wewe unaonaje?
Dakika za lala salama, Palace waliwasha moto mkali, dakika ya 90′ Glenn Murray alikosa penalti, lakini katika dakika hiyo hiyo Glenn akamalizia mpira uliookolewa na kipa Mignolet, hivyo kuandika goli la tatu.
Zaha akifunga goli la pili
Comments
Post a Comment