Simba waweka wazi ugonjwa anaoumwa katibu mkuu aliyeomba kujiuzulu


Simba waweka wazi ugonjwa anaoumwa katibu mkuu aliyeomba kujiuzulu

KABURU

UONGOZI wa Simba umethibitisha rasmi kupokea barua ya katibu mkuu wake, Stephen Ally akiomba kujiuzulu wadhifa wake kutokana na matatizo ya afya.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Erick Nyange 'Kaburu' amesema jioni ya leo: "Kweli katibu mkuu ametuandikia barua ya kuomba kujiuzulu au kuacha kazi kwa sababu za matatibu. 

Nini kinamsumbua katibu huyo? Kaburu amefafanua: "Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la koo na ndani ya siku mbili, tatu ataenda kufanyiwa upasuaji unaoweza kumuweka nje ya kazi kwa muda mrefu, kwa jinsi majukumu ya Simba yalivyo kwasasa anahitajika kufuatilia kazi za kila siku hasa kipindi hiki ligi imekwisha,  kuna masuala ya maandalizi ya msimu mpya na usajili, hivyo ameona kipindi hiki aweze kupumzika ili mtu mwingine aje kuchukua nafasi yake"

"Ni taarifa tuliyopokea kama uongozi wa juu, rais (Evans Aveva) ataitisha kikao cha kamati ya utendaji kuweza kujadiliana na baada ya hapo tutaamua nani atakuwa mbadala wake na utaratibu mzima wa kumpata katibu mkuu mpya".



Comments