SADIO MANE RAIA WA SENEGAL ANAYEWEKA HISTORIA MPYA PREMIER LEAGUE HUKU SOUTHMPTON IKIINYANYASA ASTON VILLA 6-0
Sadio Mane ameweka historia mpya kwenye Premier League baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick ) ya haraka zaidi kuliko wakati wowote ule katika ligi hiyo.
Hiyo ilikuwa ni katika mechi ya maangamizi kwa Aston Villa iliyopokea kipigo cha 6-1 kutoka kwa Southampton.
Magoli matatu ndani ya dakika mbili na sekunde 56 kutoka kwa winga huyo raia wa Senegal, lilikuwa ni jambo la kuduwaza.
Matokeo hayo yanaiweka Southampton kwenye nafasi nzuri ya kucheza Europa League msimu ujao huku Aston Villa ikisogea kwenye ukanda wa janga la kushuka daraja.
Sadio Mane alifunga magoli hayo katika dakika ya 13, 14 na 6 huku magoli mengine ya Southampton yakifungwa na Shane Long aliyefunga mara mbili pamoja Graziano Pelle wakati bao pekee la Aston Villa lilifungwa na Christian Benteke.
Sadio Mane akishangilia rekodi mpya aliyoweka Premier League
Wachezaji wa Southampton wakimpongeza Mane
Alan Hutton akishindwa kumzuia Mane asifunge bao la kwanza
Mane akitupia la pili
Bao la tatu la Mane
Comments
Post a Comment