Real Madrid wavuliwa taji la Uefa na Juventus, wachapwa 3-2



Real Madrid wavuliwa taji la Uefa na Juventus, wachapwa 3-2

1431547746091_lc_galleryImage_Football_Real_Madrid_v_Ju

REAL Madrid walihitaji ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Juventus usiku huu ili kutinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini ndoto zao zimezimwa Santiago Bernabeu.

Cristiano Ronaldo ameamusha uwanja wa mzima wa Bernabeu baada ya kufunga goli la kuongoza dakika ya 23′ kwa mkwaju wa penalti na limedumu mpaka mapumziko,  lakini Alvaro Morata amesawazisha goli hilo dakika ya 57′ akipokea pasi murua kutoka kwa Paul Pogba.

Morata ameiadhibu klabu yake ya zamani na kuunyamazisha mji wa Madrid baada ya mabingwa hao watetezi wa UEFA, Real Madrid kuvuliwa taji lao walilotwaa mjini Lisbon mwaka jana wakiifunga Atletico Madrid.
Mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Juventus mjini Turin, Juve walishinda magoli 2-1 na kutokana na sare ya leo wanatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2.
Licha ya matokeo hayo, mechi ya leo imebalansi kwa muda mrefu na timu zote zimemilikia mpira asilimia 50 kwa 50, lakini dakika za mwisho Real wameongeza asilimia za kumiliki mpira mpaka kufikia 53 kwa 47.
Juventus tangu droo ya nusu fainali ilipotoka, watu wengi waliwadharau, lakini wamefanikiwa kutinga fainali itayofanyika juni 6 mwaka huu mjini Berlin, Ujerumani dhidi ya Barcelona fc.
Barca walitinga fainali jana kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-3 dhidi ya Bayern Munich.
Mechi ya kwanza Camp Nou, Barca walishinda 3-0 na jana usiku walifungwa 3-2.

TAKWIMU ZA LEO



Comments