RAHEEM STERLING HATARINI KUTIMKA LIVERPOOL, AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE …Chelsea na Arsenal zamsubiri



RAHEEM STERLING HATARINI KUTIMKA LIVERPOOL, AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE …Chelsea na Arsenal zamsubiri
Forward Sterling has already            turned down a contract offer of £90,000-a-week
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling ameingia kwenye hatua mpya ya sakata lake la kutimka Anfield baada ya kuelezwa kuwa nyota huyo yuko njiani kutafuta changamoto mpya. 
Inadaiwa Sterling mwenye umri wa miaka 20 tayari ameweka sokoni nyumba yake iliyoko Merseyside, hali inayozidi kupalilia moto wa tetesi za kuondoka kwake.
Hatima ya Sterling Anfield imekuwa iking'ining'ia baada ya kukataa kusaini mkataba mpya hadi msimu umalizike kwanza.
Kukosa nafasi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao, kunachukuliwa kama pigo lingine kwa kocha Brenden Rodgers katika harakati zake za kuhakikisha winga wake huyo anabakia katika kikosi chake.
Arsenal na Chelsea zinahusishwa kwa karibu sana na usajili wa Raheem Sterling.
Raheem Sterling's Liverpool                  future remains in doubt with the forward stalling on a                  new contract
Hatma ya Raheem Sterling ndani ya Liverpool iko mashakani
The 20-year-old has fuelled                  talk of a move to Chelsea or Arsenal after looking for a                  property in London
Raheem Sterling anahusishwa na  Chelsea au Arsenal





Comments