Raheem Sterling amepokea tuzo yake ya mchezaji bora chipukizi wa Liverpool huku akikumbana na ushangiliaji wenye utata - wengine wakimzomea, wengine wakimshangilia.
Masaa machache baada ya kubainishwa kuwa anataka kuondoka Liverpool, nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, akakabidhiwa tuzo hiyo iliyotolewa kwenye ukumbi wa Echo Arena.
Akatoa hotuba fupi ya shukran huku baadhi ya mashabiki wakiimba "Usiondoke Raheem" lakini alipomaliza kuongea na kuanza kuondoka jukwaani baadhi ya mashabiki miongoni mwa mashabiki 3000 waliohudhuria sherehe hizo wakamziomea.
Raheem Sterling ametajwa kama mchezaji bora chipukizi wa Liverpool
Raheem Sterling akiwasili uwanja wa mazoezi wa Liverpool - Melwood training headquarters kabla ya kuelekea kwenye sherehe za tuzo za klabu hiyo
Comments
Post a Comment