WENGI tunaufahamu wimbo maarufu wa NyakoKonya wa Orchestra Mangelepa, bendi iliyokuwa ya wanamuziki waliomkimbia Baba Gaston na kuanzisha bendi yao. Mangelepa ilikuwa tishio katika Afrika ya MMashariki kwa vibao kama Embakassy, Walter, Maindusa. Lakini nimetaja Nyako Konya kwani nimemkumbuka ghafla Badibanga Wa Tshilumba Kai Kai mtunzi wa kibao hiki. Kai kai ndilo jina alilojulikana nalo sanana hata wakati akiwa kwa Baba Gaston waliwahi kutoa kibao kinaitwa Kai kai. Huyu bwana alikuwa muimbaji mahiri ambae pia alikuwa akipiga trombone kwenye bendi hii ya Mangelepa. Kai kai alikuwa mmoja wa wanamuziki waliokuwa katika kundi la Baba Gaston Ilunga wa Ilunga lililo ondoka Kongo miaka ya 70 na kuja Afrika ya Mashariki kutafuta maisha, Na walipokewa vema Dar es Salaam na bendi hiyo kurekodi nyimbo kadhaa katika studio ya TFC. Hatimae kundi hili lilihamia Nairobi na kuwa likifanya maonyesho Park restaurant iliyoko Uhuru Park, na hapo ndipo walipokuja na kibao Kakolele Viva Christmas. Lakini kama nilivyosema awali kundi zima likamkimbia Baba Ilunga na kuanzisha kundi la Les Mangelepa. Umaarufu wa Les Mangelepa ulifanya vikundi vingi vya wanamuziki wa Kongo kuhamia Nairobi , hivyo kukaweko na makundi kama
Les Kinois, Super Mazembe, and Viva Makale, Shika shika na vingine vingi na kufanya biashara kuwa ya mashindano magumu ya kimuziki, ukichukulia pia kulikuwa na bendi kama Simba wa Nyika , Les Wanyika, na bendi za Wakenya kama Maroon Comandoes, Kilimambongo Boys na kadhalika. Badibanga Wa Tshilumba Kai Kai alihamia Afrika ya Kusini kuanzia mwaka 1985. Na amefia huko February mwaka huu na kuzikwa Johanesburg. Pamoja na Nyako Konya Kai kai pia ndie mtunzi wa wimbo wa Walter, ambao aliuimba na Kalenga Vivi Nzanzi, na kabila Kabanze.
Comments
Post a Comment