Pluijm ataja kikosi bora VPL 2014/2015, nyota wa Simba watumbukia….



Pluijm ataja kikosi bora VPL 2014/2015, nyota wa Simba watumbukia….

DSC_0141

MSIMU wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara umemalizika mwishoni mwa juma lililopita (Mei 9 mwaka huu) na kushuhudia Yanga wakitangazwa mabingwa, Azam nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Mbeya City nafasi ya nne, huku Ruvu Shooting na Polisi Morogoro zikishuka daraja.

MSIMAMO MZIMA HUU HAPA

Baada ya ligi kumalizika mtandao huu unafanya utafiti ambao matokeo yake na maana nzima vitawekwa bayani siku za usoni, lakini umeanza na kujua vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu kwa msimu uliomalizika siku za karibuni.

Kila kocha anapewa nafasi ya kutaja wachezaji 11 kutoka timu zote ambao anaona wanaingia katika kikosi chake bora kabisa msimu mzima.

Leo tunaanza na kocha aliyetwaa ubingwa akiifundisha Yanga, Hans van der Pluijm ambaye amesema;

"Golini namuweka Ally Mustafa, nadhani amecheza vizuri sana, beki wa kulia ni Juma Abdul, mabeki wa katikati nawaweka Paschal Wawa na Nadir Haroub, kushoto Tshabalala kutoka Simba, sijui jina lake, najua jina lake la utani ni Tshabalala".

"Safu ya kiungo ni Said Ndemla kutoka Simba, winga ya kulia ni Msuva, winga wa kushoto Emmanuel Okwi, kiungo cha mbele Niyonzima na washambuliaji wawili ni Amissi Tambwe na Kavumbagu'.

"Sikuwepo wakati ligi inaanza, nilianza kazi Yanga mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, lakini kwa kipindi nilichoona ligi nimewaona wachezaji hao kuwa bora zaidi msimu huu".

KIKOSI BORA CHA KOCHA WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM MSIMU WA 2014/2015 NA TIMU WALIZOTOKEA WACHEZAJI HAO

  1. Ally Mustafa (Yanga)
  2. Juma Abdul (Yanga)
  3. Mohamed Hussein 'Tshabala' (Simba)
  4. Nadir Haroub (Yanga)
  5. Paschal Wawa (Azam fc)
  6. Said Ndemla (Simba)
  7. Simon Msuva (Yanga)
  8. Haruna Niyonzima (Yanga)
  9. Amiss Tambwe (Yanga)
  10. Didier Kavumbagu (Azam fc)
  11. Emmanuel Okwi (Simba)

Kesho tutakuletea kikosi bora cha kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kwhelo 'Julio', endelea kuwa nasi…..



Comments