Manchester United haitaweza kumrejesha Old Trafford kiungo wake wa zamani Paul Pogba, hii ni kwa mujibu wa kiungo mwenzake wa Juventus Andrea Pirlo.
Juventus ipo mashakani kumkosa Pobga msimu ujao huku United, Manchester City, Chelsea, Real Madrid na Barcelona zikIhusishwa na usajili wake katika dirisha la usajili la mwezi Juni.
Lakini Pirlo anasema Pobga hawezi kurejea United kwa namna walivyomfanya hadi akaamua kutimka mwaka 2012.
"Ana furaha hapa Juventus, na hata kama ataondoka basi sio kwa Manchester United," alisema Pirlo.
Pobga aliwahi kuweka hadhari kuwa hakuvutiwa na uwepo wake Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson ambapo alikosa kabisa nafasi ya kukitumikia kikosi cha kwanza.
Kiungo wa Juventus Paul Pogba amekuwa akihusishwa na safari ya kwenda Man United, Man City au Chelsea
Andrea Pirlo (kulia) anasema Pobga hawezi kukubali kurejea Manchester United
Pogba aliondoka Manchester United kama mchezaji huru 2012 baada ya kokosa nafasi kikosi cha kwanza
Sir Alex Ferguson alishindwa kumtumia Pogba kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United
Comments
Post a Comment