Picha ya wiki: Gigi Buffon aonekana kama anataka kumbusu refa mdomoni



Picha ya wiki: Gigi Buffon aonekana kama anataka kumbusu refa mdomoni
1431547793206_lc_galleryImage_Juventus_Spanish_forward_
Wachezaji wa Juventus wakishangilia jana
PICHA yenye mvuto ilitawala katika mitandao ya kijamii wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi ya marudiano ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Real Madrid na Juventus jana uwanja wa Santiago Bernabeu.
Cristiano Ronaldo iliifungia Real Madrid  goli la kuongoza kipindi cha kwanza kwa mkwaju ya penalti kufuatia James Rodgriguez kuangushwa kwenye eneo la hatari na Giorgio Chiellini.
Baada ya faulo ya Chiellini wachezaji wa Juve walimzonga mwamuzi wa Sweden, Jonas Eriksson wakijaribu kupinga maamuzi yake.
Wakati wa tukio hilo, mpiga picha mmoja mjanjamjanja alipiga picha iliyoonesha kama golikipa wa Juventus, Gigi Buffonwas alikwenda kumbusu mdomoni mwamuzi Jonas Eriksson.
Tukio hilo lilirudisha nyuma kumbukumbu za watu kuhusu ishu waliyowahi kufanya  Gary Neville na Paul Scholes enzi hizo wakiwa Manchester United.
Picha hiyo ilisambaa kwa haraka kwenye mitandao ya kijamii.
Picha yenyewe hii hapa chini


Comments