PEP GUARDIOLA AIKATA MAINI MANCHESTER CITY …asema: “Nimeshasema mara milioni 200 bado nina mkataba na Bayern Munich”
Pep Guardiola amekanusha uvumi wa kwenda kujiunga na Manchester City msimu ujao na kudai bado ana mkataba na Bayern Munich.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 ameachia habari hizo mbaya kwa mashabiki wa Manchester City kwa kusema: "Nimeshasema mara milioni 200 kuwa nina mkataba na Bayern hadi mwaka 2016. Nabakika hapa na hiyo ndiyo hali halisi."
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amesisitiza kuwa ataendelea kuwa na timu hiyo msimu ujao
Hatma ya Guardiola Bayern imekuwa mashakani
Kocha huyu wa Kihispania ameshuhudia timu take ikipoteza michezo minne mfululizo katika mashindano yote
Comments
Post a Comment