Na Anwar Binde,
Shabiki mmoja kwa jina la Ross Morgan, 25, alikuwa akitizama mechi kati ya Ipswich na Norwich jumamosi iliyopita wakati huo timu yake ikiwa nyuma kwa bao moja.
Baada ya Paul Anderson kufunga goli la kusawazisha alipata wazimu na akaruka juu na kupiga ngumi dari ya nyumba yake ikatoboka
Morgan aliipiga picha shimo hilo na akaiweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.
Mashabiki wenza waliisambaza na ikamfikia Anderson ambaye ilimgusa na akajitolea kugharamia hasara aliyosababisha.
Mchezaji huyo wa Ipswich aliwatamausha mashabiki waliokuwa wakifuatilia mazungumzo yao kwa ukarimu wake.
Morgan, aliachwa kinywa wazi na ukarimu wa Anderson.
Kwa sasa shabiki huyo mtata anapania kutizama mechi ya marudiano kati ya Ipswich na Norwich katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.
Comments
Post a Comment