PARIS St-GERMAIN MABINGWA LIGI YA UFARANSA


PARIS St-GERMAIN MABINGWA LIGI YA UFARANSA

psg

Na Anwar Binde.

Paris St-Germain wamefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu Ufaransa kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kupata ushindi dhidi ya Montpellier.

PSG walikuwa wakihitaji pointi moja tu ili kuweza kufanikiwa kunyakua taji ilo na kuwa klabu ya nne nchini Ufaransa kuweza kunyakua taji hili kwa mara tatu mfululizo.

Kiungo wa Ufaransa Blaise Matuidi aliweza kufunga goli moja pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina Ezequiel Lavezzi.

Montpeller walijibu mashambulizi kwa kufankiwa kupata bao moja lilo fungwa na mshambuliaji wao Anthony Mounier ila vijana wa Laurent Blanc waleza kulinda ushindi wao mpaka mwisho.

Baada ya ushindi huo PSG sasa wanaweza beba mataji matatu ndani ya msimu mmoja ikiwa watafanikiwa kuchukua taji la French Cup na French League Cup.

PSG walikua bila ya mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic ambaye alikua akisumbliwa na maumivu ya paja, kukosekana kwake kulibadili kidogo uchezaji na makali ya PSG kwa ujumla.

PSG katika mechi zao nne zilizopita wamekua na rekodi nzuri ya ufungaji wakifanikiwa kufunga goli 17, huku wakipata ushindi mnono dhidi ya Lille na Guingamp kwa kuweza kuwafunga goli sita kwa kila timu.



Comments