Mashabiki wameshindwa kuvumilia hali ya kusubiri mabondia kupanda ulingoni baada ya waandaji wa pambano kati ya Francis Cheka dhidi ya bondia Kiatchai Singwancha kuonekana wanachelewesha kwa makusudi mabondia waliondaliwa kuzichapa kwenye mapambano ya utangulizi kinyume na ratiba ilivyokuwa ikielekeza.
Mashabiki alimanusura waanzishe fujo kutokana na uvumilivu kuwashinda.
Mashabiki hao waliojitokeza kwa uchache wameonekana kukasirishwa na kitendo hicho na kuanza kumsaka 'promoter' wa pambano hilo lakini polisi imebidi waingilie kati kutuliza rapsha zilizotaka kutokea.
Awali ya yote, waandishi wa habari wametumia msuli kuingia kwenye ukumbi baada ya walinzi waliokuwa mlangoni kuwazuia na kudai hawatambui uwepo wao mahali hapo. Kitu hicho kiliwaudhi waandishi na wengine kuamua kususi pambano hilo na kuondoka.
Comments
Post a Comment