Nsimbe, Kitambi waongezewa ulaji Azam fc kumsaidia Stewart Hall


Nsimbe, Kitambi waongezewa ulaji Azam fc kumsaidia Stewart Hall

KITAMBI-1

Dennis Kitambi anakuwa kocha msaidizi namba mbili wa Azam fc.

KOCHA mkuu mpya wa Azam fc, Muingereza, Stewart John Hall amekubali kufanya kazi na waliokuwa makocha wa muda wa klabu hiyo, George 'Best' Nsimbe na Dennis Kitambi.

Nsimbe alirithi kwa muda mikoba ya, Mcameroon,  Joseph Marius Omog aliyefutwa kazi mwezi februari mwaka huu baada ya Azam fc kutupwa nje ya ligi ya mabingwa Afrika na El Merreikh ya Sudan, wakati Kitambi naye alichukua mikoba ya aliyekuwa kocha msaidizi, Ibrahim Shikanda.

Awali zilizuka taarifa kuwa Nsimbe na Kitambi wamepelekwa kufundisha timu ya vijana ya akademi ya Azam fc na Stewart atakuja na wasaidizi wake, lakini taarifa za uhakika ni kwamba makocha hao wawili wamesaini mikataba ya kuendelea kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya kwanza.

Nsimbe amepewa mkataba wa mwaka mmoja na anakuwa kocha msaidizi namba moja wakati kitambi naye amepewa mkataba kama huo na anakuwa kocha msaidizi namba mbili.,

Tayari Stewart ameshaanza vikao vya ndani toka jumatatu ya wiki hii na ataanza kazi rasmi juni 15 mwaka huu pamoja na wasaidizi wake hao



Comments