Mwadui fc wailiza Kagera Sugar, wachukua bonge la mchezaji


Mwadui fc wailiza Kagera Sugar, wachukua bonge la mchezaji
mwanga
Mwanga (kushoto) akisaini mkataba Mwadui fc
WIKI chache baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom, timu ya Mwadui Fc iliyoapanda ligi kuu kwa msimu ujao wa 2015-2016 imeanza kuboresha kikosi chake.
 
Timu hiyo kutoka  mkoani Shinyanga imeanza kwa kukamilisha usajili wa aliyekua Nahodha wa timu ya Kagera Sugar, MalegesI Samuel Mwanga.
 
Mwenyekiti wa timu hiyo Joseph Kaasa amesema kwamba wamejipanga kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya 30 ili kuunda kikosi cha ushindani na ikibidi kutwaa ubingwa  msimu ujao.
  Kwa upande wake  Mwanga amewaomba  mashabiki wa soka wa timu hiyo kumpa sapoti kwani anatarajia kufanya mambo mazuri Mwadui Fc .
 
MalegesI alianza soka lake katika timu ya Kagera Sugar ikiwa daraja la kwanza mwaka 2005 kisha akaenda kucheza soka la kulipwa falme za kiarabu kabla ya kurejea na kujiunga na timu ya Azam Fc mwaka 2010 alikodumu kwa mwaka mmoja.
Baada ya hapo alirejea timu ya kagera na kukabidhiwa unahodha hadi leo alipojiunga na Mwadui Fc.


Comments