MUZIKI HAUNA UMRI, HEBU MCHEKI HUYU BABU ALIVYOCHENGUKA NA GOMA LA MASHAUZI CLASSIC TCC CLUB CHANG’OMBE
Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa TCC Club Chang'ombe kulikuwa na onyesho la Mashauzi Classic ambapo kamera ya Saluti5 ilivutiwa na 'babu' huyu ambaye jina lake halikuweza kupatikana.
Bwana mkubwa huyu alikuwa miongoni mwa watu wachache waliokuwa wabishi na kwenda kuhudhuria onyesho hilo lililosindikizwa na mvua mchana kutwa, usiku kucha na kusababisha maonyesho mengi kuahirishwa.
Babu akaonyesha jinsi gani muziki upo kwenye damu ambapo alicheza mdadi kuanzia kaunta hadi jukwaani kwa wasanii. Akacheza na kila aliyekuja mbele yake.
Babu akiwa eneo la kaunta akiyarudi mangoma
Babu anaendelea kusakata muziki na mrembo aliyekumbana nae hapo hapo TCC Club
Mpaka chini
Babu anaonyesha mbwembwe zake
Hapa yuko na patna mwingine
Sasa yuko jukwaani
Ana nena la moyoni kwa mwimbaji
Babu anaambiwa inatosha wacha watu wafanye kazi zao











Comments
Post a Comment