GAZETI la leo jumapili la            The Sun limechapisha stori maalumu kutoka kwa vyanzo            vya karibu vya Mwanamitindo maarufu wa Urusi, Irina Shayk             ambaye alivunja uhusiano wa mapenzi dhidi ya nyota wa Real            Madrid, Cristiano Ronaldo.
        Hata hivyo The Sun            limeshindwa kujaa na nukuu kutoka kwa wawili hao (Ronaldo na            Irina).
        Mwanamitindo wa Urusi            Shayk na 'supastaa' wa Real Madrid, Ronaldo walikuwa na            mahusiano ya mapenzi kwa miaka mingi, lakini mahusiano yao            yalivunjika mwanzoni mwa mwaka huu.
        Irina Shayk kutoka hapo            ana mahusiano na mwigizaji wa  Hollywood, A-lister Bradley            Cooper na anaonekana kufurahia mapenzi yao.
        Lakini sasa ameamua            kumwaga mchele akieleza kilichomfanya aachane au ampige chaga            Ronaldo.
        Kwa mujibu wa gazeti hilo            la udaku, Cristiano Ronaldo alimsaliti Irina Shayk kwa            kutembea na 'dazani' ya wanawake, yaani Ronaldo alizidi kuwa            na michepuko.
        Wakieleza zaidi namna            Irina alivyobaini, The Sun wanasema Cristiano alikuwa            anachati na wanawake wengi mno ambao walibainika kuwa wapenzi            wake au michepuko yake na hali hii  ikaamusha hasira za Irina.
        Sasa imefahamika kwa            mujibu wa ripoti ya The Sun kuwa Ronaldo ndiye            aliachwa na Irina Shayk na sio yeye kumuacha mwanamitindo            huyo.
        Tazama nakala ya gazeti            la The Sun chini likieleza stori hiyo
        
Comments
Post a Comment