Real Madrid imejitosa kwenye mazoezi kabambe kujiandaa na mechi ya marudiano ya nusu faina ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus huku misuli ya Cristiano ikiwa kivutio kikubwa.
Real Madrid inawakaribisha Juventus kwenye dimba la Santiago Bernabeu huku wakiwa na deni la bao 1-0 walilotunguliwa kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita.
Mbali na kusaka tiketi ya kwenda fainali, Ronaldo pia atakuwa kwenye ligi nyingine ya ushindani wa kufunga magoli mengi katika Champions League kati yake na Lionel Messi wa Barcelona ambaye anaongoza kwa tofauti ya goli moja.
Ronaldo alionekana mazoezi huku akiwa kwenye hali ya ukakamavu iliyoonyesha misuli yake iliyojengeka vilivyo.
Ronaldo akiwa mazoezini na wachezaji wenzake kwenye uwanja wa Valdebebas Jumanne asubuhi
Dani Carvajal, Lucas Silva, Fabio Coentrao na Ronaldo (kushot kwenda kulia) wakiwa mazoezini kujiandaa na Juventus

Comments
Post a Comment