Mashindano ya mpira wa kikapu yanayoshirikisha majiji ya Afrika Mashariki na Kati yamezidi kushika kasi, michuano hiyo imeendelea tena leo kwa michezo minne kupigwa kwenye uwanja wa Taifa wa ndani ikiwa bado mi hatua ya makundi.
Mchezo wa kwanza kwa siku ya leo ulikuwa kati ya Dar City dhidi ya Tanga, mhezo huo ulimalizika kwa Dar City kuibuka na ushindi baada ya kuibugiza Tanga kwa jumla ya vikapu 59 kwa 46. Mchezo mwingine ulizikutanisha timu ya Mogadishu City na Mbeya ambapo Mbeya wameshinda mchezo huo kwa vikapu 71 kwa 59 vya Mogadishu City.
Mchezo wa tatu ulizikutanisha timu za wanawake ambapo Kampala ilikuwa ikichuana na Nairobi, mchezo huo ulimalizika kwa timu ya Nairobi kuigaragaza Kampala kwa kuitandika vikapu 71 kwa 55. Nairobi City imeshashinda michezo yake miwili baada ya jana kuiangushia kichapo timu ya Dar City kwa vikapu 83 kwa 42.
Dar Stars walipambana na timu ya Cairo kutoka Misri kwenye mchezo ambao Dar City walionekana kuzidiwa kwa kilakitu na timu ya Cairo. Mchezo huo umemalizika kwa Dar City kukubali kichapo cha vikapu 81 kutoka kwa Cairo wakati wao wakiwa wamefunga vikapu 51.
Kesho michuano hiyo itaendelea tena kwa mechi nne kupigwa, timu ya Nairobi itacheza dhidi ya Dar City (kwa upande wa wanawake) wakati wakati kwa upande wa wao wataingia moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali. Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya Cairo ya Misri dhidi ya Dar City wakati Qardo ya kutoka Somalia itacheza na Dar Star kwenye nusu fainali ya pili.
Mchezo wa fainali utapigwa siku ya jumapili.
Comments
Post a Comment