Ligi kuu ya Hispania sasa itaweza kuendelea tena wikiendi hii baada ya kusitishwa kwa wiki nzima na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Hispania (Spanish Football Federation – RFEF) na mgomo wa wachezaji kuisha.
Baada ya Mahakama Kuu ya Hispania kusema kuwa mgomo wa wachezaji kuhusu haki za televisheni si halali/si wa kisheria (unlawful), Shirikisho nalo lilibadilisha kauli yake kwamba 'msimu umeisha'
Barcelona inaweza kushinda taji la La Liga Jumapili hii, kabla mechi ya mwisho haijachezwa, endapo itawafunga mabingwa, Atletico Madrid.
Mechi ya Kombe la Mfalme nayo itachezwa kama ilivyopangwa, tarehe 30 Mei. Barca – ambao pia wamefikia fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, watakayovaana na kibibi kizee cha Turin, Juventus – watacheza na Athletic Club Bilbao kwenye Uwanja wa nyumbani, Camp Nou kwenye fainali hiyo ya Kombe la Mfalme.
Mwandishi habari za soka nchini Hispania, Andy West anaelezea mgogoro huu:
"Kimsingi, usitishwaji wa ligi ulikuwa ni matokeo ya vita ya madaraka juu ya nani anaendesha mpira wa Hispania. Ni dhahiri kabisa, hiki ni kilele cha mgogoro wa muda mrefu juu ya mgawanyo wa mapato ya televisheni ambayo yamekuwa yakipimwa kwa kuwapendelea 'wakubwa wawili' wa Barcelona na Real Madrid."
Shirikisho na umoja wa wachezaji (AFE) zimeridhika na sheria mpya inayojumuisha majadiliano ya bei juu ya haki za televisheni kwa mechi za ndani , inayoungwa mkono pia na wasimamizi wa Ligi ya Mpira wa Kulipwa nchini humo (National Professional Football League – LFP), inayoendesha ligi mbili kubwa za kulipwa nchini humo.
Wachezaji waliounga mkono mgomo wanaamini mgawanyo wa pesa kwenye mkataba mpya uliopendekezwa na LFP na serikali ya Hispania hauwanufaishi wale wanaozichezea klabu za chini/ ndogo.
Ijumaa iliyopita, Raisi wa LFP, Javier Tebas alitangaza mipango ya kwenda mahakamani dhidi ya usitishwaji wa ligi, huku akionya italeta hasara ya mapato hadi € 50 milioni (zaidi ya bilioni mia, shilingi za Tanzania) kwa mechi za mzunguko mmoja.
Hii Ndio Ratiba ya Mechi Kali Zilizobaki Hispania.
Jumapili, 17 Mei: Atletico Madrid v Barcelona
Espanyol v Real Madrid
Jumamosi, 23 Mei: Barcelona v Deportivo
Real Madrid v Getafe
Jumamosi, 30 Mei: Fainali ya Kombe la Mfalme
Athletic Bilbao v Barcelona
Comments
Post a Comment