MEMPHIS DEPAY AFUZU VIPIMO VYA AFYA MANCHESTER UNITED



Memphis Depay amepigwa picha akiondoka uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Aon Training Complex baada ya kukamilisha vipimo vya afya kwa klabu yake mpya.
Winga huyo wa Holland ambaye ni usajili wa kwanza wa United kwa msimu ujao, aliwasili kwenye mji wake mpya Jumatatu kwaajili ya hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake.
United imeandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Depay amefuzu vipimo vya afya na sasa wanasubiri kukamilisha usajili wake pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi ujao.
Depay mwenye umri wa miaka 21 anajiunga na United baada ya msimu wa mafanikio akiwa na PSV ambapo alifunga magoli 22 katika mechi 30 alizocheza.
Memphis Depay (circled) leaves Manchester United's                Aon Training Complex after his medical on Monday
Memphis Depay (kwenye kiduara) akiondoka  Aon Training Complex baada ya kukamilisha vipimo vya afya
Depay                flew into Manchester on Monday to put the finishing                touches to his transfer from PSV Eindhoven
Depay alipaa kwenda Manchester Jumtatu kwaajili ya kukamilisha usajili wake kutoka PSV Eindhoven
The                Holland winger leaves United's training ground in a car                driven by a club official on Monday afternoon






Comments