MATS HUMMELS ARUDI TENA KWENYE RADA ZA MANCHESTER UNITED


MATS HUMMELS ARUDI TENA KWENYE RADA ZA MANCHESTER UNITED
Mats Hummels ameripotiwa kujiandaa kucheza mechi ya mwisho akiwa na Borussia Dortmund kabla ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United.
Kwa mujibu wa gazeti la Star, beki huyo wa kati raia wa Ujerumani atacheza fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Wolfsburg na ana matumaini ya kubeba taji lake la mwisho kabla ya kuondoka.
Dortmund imebariki kuondoka kwa beki huyo na mtendaji wake mkuu, Hans Joachim Watzke amekiri kuwa hawana shida juu ya kuwapiga bei wachezaji wao nyota.



Comments