MATS HUMMELS AITOLEA NJE MANCHESTER UNITED …Van Gaal sasa amtaka Nicolas Otamendi wa Valencia, Jonny Evans kutimkia Everton
Imedaiwa kuwa sentehafu wa kimataifa wa Ujerumani, Mats Hummels hana mpango wa kujiunga na Manchester United na badala yake anataka kubaki Borussia Dortmund.
Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc ameliambia gazeti la Kicker la Ujerumani kuwa beki huyo mwenye thamani ya pauni milioni 37 hataondoka.
Badala yake United sasa inafufua msako wa kumnyakua beki wa Valencia Nicolas Otamendi mwenye umri wa miaka 27 kwa pauni milioni 36.
Otamendi beki wa kimataifa wa Argentina aliwaniwa na United dirisha la Januari lakini dili halikuiva.
Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amebaini tatizo kwenye safu yake ya ulinzi ambapo Phil Jones, Jonny Evans na Marcos Rojo wote wameshindwa kuwa na nafasi ya kudumu.
Aidha, Evans pia inadaiwa yuko njiani kutimka Old Trafford huku ikisemekana Everton wanaelekea kushinda mbio za kumnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 27.
Mats Hummels amechomoa kujiunga na Manchester United na kuamua kubaki Dortmund
Sentahafu wa kimataifa wa Ujerumani sasa kubakia Dortmund msimu ujao
Manchester United sass inamsaka Nicolas Otamendi wa Valencia
Jonny Evans njiani kujiunga na Everton
Comments
Post a Comment