Marefa wanne wa Tanzania wachaguliwa kuchezesha kufuzu Afcon 2017



Marefa wanne wa Tanzania wachaguliwa kuchezesha kufuzu Afcon 2017

NKONGO
WAAMUZI wanne (4) wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la soka barani Afrika, CAF,  kuchezesha mechi namba 8 ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, Afcon 2017 baina ya Uganda na Botswana.

Mwamuzi wa kati katika mechi hiyo itayopigwa Juni 13 mwaka huu mjini Kampala, Uganda, ameteuliwa Mtanzania Israel Mujuni Nkongo.

Watanzania wengine watakaochezesha mechi hiyo na nafasi zao kwenye mabano ni John Longino Kanyenye (mwamuzi msadizi namba moja), Josephat Deu Bulali (mwamuzi msaidizi namba mbili) na Martin Eliphas Sanya (mwamuzi wa akiba).

Kamishina wa mechi hiyo atakuwa Julius Elly O. Mukolwe kutoka Kenya.



Comments