Imedaiwa kuwa Manchester United wanataka walipwe na Real Madrid pauni milioni 29 ili kumwachia kipa David de Gea.
Imeripotiwa kuwa De Gea amekubaliana na Real Madrid juu ya maslahi yake binafsi katika dili linalotajwa kufikia zaidi ya pauni milioni 3.6 kwa mwaka, lakini miamba hiyo ya Hispania bado haijakubaliana na Manchester United juu ya usajili wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amebakiza miezi 14 ya mkataba wake Old Trafford.
Gazeti la Marca la Hispania limedai United inataka pauni milioni 28.6 kwa kipa huyo kwa kimataifa wa Hispania lakini pia kukiwa na sharti la kupewa beki wa kushoto Fabio Coentrao.
David de Gea akiaminika kuwa alikuwa anawaaga mashabiki wa Manchester United katika mchezo dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita
De Gea akiwapungia mashabiki wakati akienda benchi baada ya kuumia
Beki wa Kireno Fabio Coentrao (katikati) anahusishwa katika dili la De Gea.
Comments
Post a Comment