MANCHESTER UNITED ‘YANASA’ KIPA KINDA MATATA KUTOKA UBELGIJI



MANCHESTER UNITED 'YANASA' KIPA KINDA MATATA KUTOKA UBELGIJI

Manchester United imemnasa kipa kinda Ilias Moutha Sebtaoui kutoka Ubelgiji ambaye alikuwa anawaniwa na timu kibao.
United imekidhi vigezo na kukubaliana na Kipa huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia anaweza akaichezea timu ya taifa ya Morocco.
Ilias Moutha Sebtaoui atajiunga na United akitokea Standard Liege huku timu kama Roma, Chelsea, Tottenham, Anderlecht na Newcastle zikiambulia patupu katika kusaka saini ya mlinda mlango huyo.
Ilias aliiwakilisha Ubelgiji katika michuano ya vijana chini ya miaka 15 na 16.
Kipa huyo anaungana na kinda mwingine wa Ubelgiji Indy Boonen ambaye alitua Old Trafford tangu mwezi Februari.
Hadi sasa United tayari ina wachezaji wawili nyota kutoka Ubelgiji Marouane Fellaini na Adnan Januzaj.




Comments