Manchester United iko tayari kuanza mazungumzo na klabu ya Sevilla kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Carlos Bacca utakaogharimu pauni milioni 21.3.
Mshambuliaji huyo raia wa Colombia alipiga mabao mawili katika fainali ya Europa League kuiwezesha Sevilla kutwaa taji.
Kwa mujibu wa mtandao wa Fichajes.net, Roma na AC Milan pia zinautamani mtambo huo wa mabao, lakini United ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kukamilisha dili.
Carlos Bacca alliwezesha Sevilla kushinda Europa League Jumatano iliyopita
Bacca akibusu kombe Europa League baada ya Sevilla kuifunga Dnipro 3-2 katika fainali iliyochezwa Warsaw
Bacca alifunga mara mbili dhidi ya Dnipro
Bacca akiifungia Sevilla bao la ushindi kwenye fainali ya Europa Legue
Bacca akifanya vitu vyake
Bacca huenda akaenda kurithi mikoba ya Mcolombia mwenzake Radamel Falcao ndani ya Old Traffod
Comments
Post a Comment