Manchester United imeambiwa isahau kabisa kuhusu kipa wa Ajax Jasper Cillessen kwani haitampata kwa bei yoyote.
United bado haijapokea ofa kutoka kwa Real Madrid kuhusu David de Gea lakini kipa wa kimataifa wa Holldan Cillessen amekuwa akijadiliwa sana wiki hii Old Trafford.
Hata hivyo mkurugenzi wa michezo wa Ajax Marc Overmars ambaye ni mchezaji wa zamani wa Arsenal, amesema Cillessen hauzwi sio kwa pauni milioni 18 tu zinazotajwa kuandaliwa na United, bali hauzwi hata kwa pauni milioni 25.
Manchester United imeambiwa isahau kuhusu kipa huyu Jasper Cillessen wa Ajax
Cillessen anafahamika vizuri kwa Louis van Gaal tangu alipokuwa nae kwenye World Cup na kikosi cha Holland
'
Comments
Post a Comment