Kwa mashabiki wa Manchester United waliokuwa wakifuatilia mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madirid na Juventus kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu Jumatano usiku, watakuwa wamefahamu ni kitu gani wanakikosa kwa kiungo Paul Pogba.
United walimuona kiungo huyo bado hana nafasi katika kikosi cha kwanza na matokeo yake akaondoka bure mwaka 2012 na sasa anatinga fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Juventus.
Pobga aliambiwa awe mpole Old Trafford: "Muda wako utawadia" hiyo ilikuwa ni meseji kutoka kwa kwa makocha wa United wakimtaka asiondoke lakini haikusaidia.
Juventus hawakuwa kwenye kiwango chao bora katika mchezo huu ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini Pobga aliyekuwa anarejea kutoka kwenye maumivu yaliyomweka nje kwa miezi miwili, aling'ara vilivyo.
Paul Pogba (kulia) akishangila na Claudio Marchisio
Pogba akidhibitiwa na Daniel Carvajal
Pogba akimjaribu kipa wa Real Madrid Iker Casillas
Comments
Post a Comment