Manchester United inaangalia uwezekano wa kumsajili kiongozi mzoefu wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger.
Imebainika kuwa kocha wa United Louis van Gaal anaamini mchezaji huyo wa kimataifa ataongeza uzoefu kwenye kikosi chake katika safu ya kiungo.
Inadaiwa kuwa tayari mazungumzo yameshaanza kati ya pande hizo mbili tangu mwezi uliopita na inaamika Schweinsteiger yupo tayari kusaka changamoto mpya.
Staa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger (katikati) anawaniwa na Manchester United
Louis van Gaal anaamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ataongeza uzoefu kwenye safu ya kiungo
Boss wa Manchester United alifanya kazi na Schweinsteiger wakati alipokuwa akiifundisha Bayern Munich
Comments
Post a Comment