Arsenal imelazimisha sare ya 1-1 kwa Manchester United katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Old Trafford.
Hata hivyo matokeo hayo yanazima njozi za Arsenal kumaliza katika nafasi ya pili ambayo sasa inakwenda kwa Manchester City.
United walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ander Herrera kunako dakika ya 30 lakini Arsenal ikachomoa dakika ya 82 kwa bao la kujifunga kupitia kwa Tyler Blackett aliyebabatuizwa na shuti la Theo Walcott.
United iliidhibiti vizuri Arsenal katika kipindi cha kwanza lakini ikawa kwenye wakati mgumu kipindi cha pili hususan baada ya mabadiliko ya kuwatoa Falcao, Rojo na De Gea aliyeumia huku nafasi zao zikichukuliwa na Van Persie, Tyler Blackett na Victor Valdes.
Herrera akishangilia bao lake Old Trafford
Marouane Fellaini (kushoto) na Ashley Young (kulia), ambao wote walichangia goli wakishangilia pamoja na Herrera
Theo Walcott akipiga krosi iliyombabatiza Tyler Blackett na kuzaa bao la kusawazisha kwa Arsenal
Walcott akishangilia goli la Arsenal
Comments
Post a Comment