MANCHESTER CITY YAIKATA MAINI ARSENAL NAFASI YA PILI …yailaza Swansea, Wilfried Bony ailiza timu yake za zamani
Manchester City imeichapa Swansea 4-2 na kupunguza kabisa matumaini ya Arsenal kushika nafasi ya pili.
Kwa ushindi huo City inafikisha pointi 76 huku ikiwa imebakiza mchezo mmoja, Arsenal ni ya tatu ikiwa na pointi 70, ikishinda michezo yake miwili iliyobakia itafikisha pointi 76.
Magoli ya City yalifungwa na Yaya Toure aliyefunga mara mbili dakika ya 21 na 74, James Milner dakika ya 36 na Wilfried Bony ambaye nusu ya msimu huu aliichezea Swansea akafunga dakika ya 90.
Swansea ilipata magoli yake kupitia kwa Gylfi Sigurdsson dakika ya 45 na Bafetimbi Gomis dakika ya 64.
Swansea ilipata magoli yake kupitia kwa Gylfi Sigurdsson dakika ya 45 na Bafetimbi Gomis dakika ya 64.
Comments
Post a Comment