Mama mzazi wa mshambuliaji Radamel Falcao amesema mwanae hana furaha Manchester United na huenda akaondoka baada ya msimu kumalizika.
Mama huyo Carmenza Zarate, amesema mwanae hana furaha lakini anaheshimu maamuzi ya kocha Louis van Gaal yaliyomwezesha kucheza kwa dakika 90 katika mechi tano tu tangu ajiunge na timu hiyo kwa mkopo.
Mshambuliaji huyo wa Colombia amefunga mara nne tu katika michezo 28 aliyocheza na kusababisha kulaumiwa sana na mashabiki wa United.
Radamel Falcao yuko njia panda
Falcao alitokea bench kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace
Falaco amecheza kwa dakika 90 katika mechi tano tu
Comments
Post a Comment